IQNA

Markel: Waislamu ni sehemu ya jamii ya Wajerumani

17:19 - January 13, 2015
Habari ID: 2706291
Kansela wa Ujerumani Bi Angela Markel amesema kuwa, Waislamu wanaoishi nchini humo ni .miongoni mwa jamii ya Wajerumani

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Ahmet Davutoglu Waziri Mkuu wa Uturuki, Bi Angela Markel amesisitiza kwamba, yeye ni Kansela wa wananchi wote wa Ujerumani bila kujadili dini na itikadi zao. Markel amesema kuwa, anaunga mkono rai na mtazamo wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Christian Wulff aliyesema mwaka 2010 kwamba, Uislamu na Waislamu ni sehemu ya Ujerumani. Kansela wa Ujerumani amesisitiza kwamba, kuna haja ya kuweko mazungumzo baina ya dini mbalimbali. Wakati huo huo, miji kadhaa ya Ujerumani jana ilishuhudia maandamano makubwa ya kulaani na kupinga uenezaji chuki dhidi ya dini ya Kiislamu unaofanywa na kundi la kufurutu ada la Pegida.../mh

2703944

captcha