Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wanawake na wasichana hao wamechaguliwa
katika mashindano ya mchujo yaliyoandaliwa na Kamati ya Kuwatuma Wasomaji
Qur'ani katika Mashindano ya Kimataifa.
Baada ya mchujo huo Bi. Zahra Qurbani ametajwa kuwa wawakilishi wa Iran
katika mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani nchini Jordan.
Aidha Bi. Zeinab Mohammadnejad atawakilisha Iran katika mashindano ya
kimataifa ya Qur'ani yatakayofanyika mjini Tehran mwezi Aprili.
Mashindano hayo ya Qur'ani ya wanawake mjini Tehran yatafanyika samamba
na Mashindano ya 34 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran.
3462268