IQNA

Kijana Mbangladeshi ahifadhi Qur'ani kwa muda wa siku 86

16:47 - October 18, 2017
Habari ID: 3471221
TEHRAN (IQNA)-Kijana mwenye umri wa miaka 11 nchini Bangladesh amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu kwa muda wa siku 86.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Yaseen Irfan ambaye yuko katika darasa la siku alianza kuhifadhi Qur'ani Tukufu mwaka jana.

Alikuwa anajitahidi kuhifadhi kurasa saba za Qur'ani kila siku sambamba na kurudia kusoma kurasa aliziokuwa wamehifadhi siku iliyotanguliwa. Kufuatia mafanikio hayo, Irfan ameenziwa katika sherehe zilizo fanyika katika Kituo cha Kuhifadhi Qur'ani cha IQRA.

Akizungumza katika hafla hiyo qarii mashuhuri wa Bangladeshi ambaye pia ni mkuu wa taasisi hiyo Ustadh Ahmed Bin Yusuf amesema amesafiri katika nchi nyingi duniani na kuhudhiria mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa miaka mingi sasa lakini hajawahi kuona kijana mwenye kipaji kama Irfan.

Amesema Yaseen Irfan ni chanzo cha fakhari kwa mji wake wa Cox's Bazar na nchi nzima kwa ujumla.

Bangladesh ni nchi ya Kusini Mashariki mwa Asia ambapo ni jambo la kawaida kuwaona vijana wakiwa wamehifadhi Qur'ani.

3652590/

captcha