IQNA

Sheikhe Mkuu wa Al Azhar aalikwa mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu mjini Tehran

9:45 - November 28, 2017
Habari ID: 3471286
TEHRAN (IQNA)-Sheikhe Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri, Sheikh Ahmed el-Tayeb amealikwa kuhudhuria Mkutanowa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu utakaofanyika wiki ijayo mjini Tehran, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mwaliko huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu Ayatullah Muhsin Araki alipokutana na Yassir Othman, msimammizi wa Idara ya Maslahi ya Misri mjini Tehran.

Kongamano hilo la 31 la umoja wa Kiislamu limeandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu na litafanyika kuanzia DIsemba 5-7.

Mkutano huo hufanyika kila mwaka kwa munasaba wa Wiki ya Umoja wa Kiislamu. Inafaa kuashiria hapa kuwa Wiki ya Umoja wa Kiislamu ni kipindi cha kati ya tarehe 12 na 17 za Mfunguo Sita Rabiu Awwal kipindi ambacho kinasadifiana na kuadhimisha Maulidi na kumbukumbu ya kuzaliwa Bwana Mtume SAW. Kuhusiana na kuzaliwa Bwana Mtume SAW kuna riwaya mbili mashuhuri. Waislamu wengi wa madhehebu ya Kisuni wanaamini kwamba, Bwana Mtume SAW alizaliwa tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal mwaka wa tembo uliosadifiana na mwaka 570 Miladia.

Kundi jengine la Waislamu ambalo linaundwa zaidi na Waislamu wa madhehebu ya Shiia Ithanaashari linaamini kwamba, Mtume wa Uislamu alizaliwa tarehe 17 Mfunguo Sita Rabiul Awwal mwaka huo huo. Mitazamo hiyo miwili takribani pengo lake ni kipindi cha wiki moja. Kwa kuzingatia hali hiyo, Imam Ruhullah al-Musawi al-Khomeini (MA) Mwasisi na Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akakitaja kipindi hiki cha wiki moja kuwa Wiki ya Umoja, ili Waislamu badala ya kuvutana na kuanza kukuza tofauti za tarehe za kuzaliwa Bwana Mtume SAW wakae pamoja na kujadili umuhimu wa umoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili Waislamu na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.Sheikhe Mkuu wa Al Azhar aalikwa mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu mjini Tehran

3667378

captcha