IQNA

Mwanasiasa aliyekuwa na chuki na Uislamu nchini Ujerumani asilimu

20:20 - January 24, 2018
Habari ID: 3471370
TEHRAN (IQNA)-Arthur Wagner, mwanasiasa aliyekuwa chuki dhidi ya Uislamu amebadili msimamo ghafla na kutangaza kuwa amesilimu na hivyo kuukumbatia Uislamu katika maisha .

Wagner ambaye alikuwa mwanachama mwandamizi wa chama cha mrengo wa kulia chenye chuki na Uislamu cha Mbadala kwa ajili ya Ujerumani-Alternative for Germany-(AfD) amesilimu na kuwashangaza wengi katika duru za mirengo yenye misimamo ya kufurutu mpaka na chuki dhidi ya Uislamu nchini Ujerumani.

Chuki dhidi ya Uislamu ni moja ya misingi ya chama cha Alternative for Germany kiasi kwamba kwenye ukurasa wa mbele wa tovuti ya chama hicho imeandikwa: 'Sisi tunaunga mkono utamaduni unaotawala Ujerumani; na kwa mtazamo wetu Uislamu hauna mfungamano na Ujerumani.'

Wagne ambaye ni naibu mwenyekiti wa  AfD katika eneo la Havelland amekataa kutoa tamko kuhusu uamuzi wake na kusema hilo ni suala binafsi. Amesema hivi karibuni alijiuzulu kutoka bodi ya  AfD katika jimbo la Brandenburg huku akisisitiza kuwa anaunga mkono haki ya katiba ya uhuru wa kuabudu.

Chama cha AfD ni cha tatu kwa ukubwa Ujerumani baada ya kushinda asilimia 12.6 ya viti katika uchaguzi wa Septemba 24.

Inafaa kuashirikia hapa kuwa asilimia 5 ya Wajerumani ambao ni sawa na watu milioni 4 wa nchi hiyo ya Ulaya yenye jumla ya watu wapatao milioni 80 ni Waislamu.

/3685075/

captcha