IQNA

Wanafunzi 200 waliohifadhi Qur'ani wahitimu Mauritania

12:36 - May 17, 2018
Habari ID: 3471517
TEHRAN (IQNA)- Mahafali ya kuhitumu wanafunzi 200 waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu yamefanyika katika Kituo cha Kufunza Kiarabu na Sayansi za Kiislamu nchini Mauritania.

Sheikh Abdul Rahman Walad Hadan mkurugenzi na muasisi wa kituo hicho amesema kilianzishwa miaka 11 iliyopita kikiwa na wanafunzi sita tu.

Ameongeza kuwa hivi sasa kituo hicho kina zaidi ya wanafunzi 300 wanaosoma katika vitengo vitatau tafauti na kwamba miongoni mwa wanafunzi 200 waliohifadhi Qur'ani 50 walikuwa ni wasichana.

Mohammad Walad Aslamo, akiwakilisha wazazi katika mahafali hayo, aliwashukuru wasimamizi wa kituo hicho na kusema wazazi wengi wamejifunza Uislamu kutoka kwa watoto wao waliohitimu katika chuo hicho.

Kituo hicho kina matawi matatu katika miji ya Nouakchott, Rosso na Boghe na kina mpango wa kuwalea wanafaunzi 600 waliohifadhi Qur'ani kikamilifu katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi katika eneo la Maghreb la magharibi-kaskazini mwa Afrika. Nchi hiyo inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 4 ambao takribani wote ni Waislamu. Nchi hiyo ni maarufu kwa harakati zake za Qur'ani.

3714856

captcha