IQNA

Idadi ya wanaokumbatia Uislamu yaongezeka Norway

10:25 - September 27, 2018
Habari ID: 3471693
TEHRAN (IQNA)- Idadi ya watu wanaokumbatia dini tukufu ya Kiislamu nchini Norway inazidi kuongezeka ambapo katika miaka ya hivi karibuni Wanorway wasiopungua 3000 wamesilimu.

Kwa mujibu wa utafiti wa Kitengo cha Utafiti wa Utamaduni na Lugha za Ulimwengu wa Mashariki katika Chuo Kikuu cha Oslo, idadi ya Wanorway wanaosilimu imekiuwa ikiongozeka kutoka muongo wa tisini.

Amesema idadi ya waliosilimu katika muongo wa 90 ilikuwa ni karibu 500 na katika miaka ya hivi karibuni idadi hiyo imefika 3,000.

Ripoti hiyo imebaini kuwa katika miaka ya nyuma aghalabu ya waliokuwa wakisilimu walikuwa ni wanawake wa Norway ambao walikuwa wanaolewa na wanaume Waislamu lakini hivi sasa idadi kubwa wanasilimu kufuatia utafiti kuhusu Uislamu.

Bi.Monica Salmout ameliambia gazeti la Verdens Gang kuwa aliukumbatia Uislamu maishani miaka minne iliyopita baada ya kufanya utafiti na kusoma vitabu kadhaa ambavyo vilimuongoza.

Salmouk anasema baada ya utafiti wake hatimaye alifika katika Msikiti wa Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu mjini Oslo na kusilimu.

Naye Solva Nabila Sexelin anasema aliamua kusilimu kutokana na tabia na maadili meme ya wakimbizi Waislamu aliokuwa akiwasaidia.

3466824

captcha