Duru za habari Palestina zinadokeza kuwa ndege zisizo na rubani zililenga barabara ya Salah al-Din, ambayo ni barabara kuu ya Gaza, mapema Jumapili.
Hujuma hiyo imekuja masaa kadhaa baada ya ripoti kusema kuwa Wapalestina wengine 11 wamejeruhiwa wakati wa shambulio la utawala huo dhidi ya maandamano katika eneo la pwani ya Ghaza.
Wizara ya afya ya Ghaza imesema Wapalestina walijeruhiwa baada ya jeshi la Israeli kuanza kuwapiga risasi waandamanaji katika sehemu ya mashariki mwa pwani ya Ghaza.
Ukanda wa Ghaza umekuwa chini ya mzingiro wa mara kwa mara wa Israeli na uchokozi unaofanana tangu 2007, wakati harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina ya Hamas ilipochaguliwa kidemokrasia kuongoza eneo hilo.