Kwa mujibu wa tovuti ya qafqn.org, duru ya nne mafunzo hayo kuhusu ‘saut’ na ‘lahn’ yanafanyika kwa njia ya intaneti.
Rasha al Turfi, naibu mkuu wa kitengo cha wanawake katika kituo hicho amesema kutakuwa na vikao viwili vya darsa kila wiki kw amuda wa miezi mitatu.
Amebaini kuwa wanafunzi 500 walijisajili kushiriki katika wa kozi hiyo ya Qur’ani kutoka Iraq na maeneo mengine duniani. Baada ya mchujo, hatimaye wanafunzi 360 walichaguliwa kushiriki katika somo hilo.