Waandamanaji hao ambao walistahimili mvua, walipeperusha bendera za Palestina na kushikilia mabango ya kulaani uvamizi wa kijeshi wa Israel dhidi ya Gaza. Walitoa wito wa kukomeshwa kwa kuzingirwa kwa Gaza. Baadhi ya mabango yalisomeka: "Komesha mauaji ya kimbari", "Nasimama na Gaza" na "Komesha uhalifu wa Israel".
Baada ya Sala, waandamanaji walitoa nara kama vile "Palestine Huru, Huru", "Komesha kuzingirwa Gaza sasa" na "Sitisha mapigano sasa". Pia wameitaka serikali ya Marekani kusitisha usaidizi wake wa kifedha na kijeshi kwa Israel.
Maandamano hayo yalienda sambamba na kusambaratika kwa mapatano ya wiki moja ya usitishaji vita kati ya utawala wa Israel na Hamas siku ya Ijumaa.
Utawala haramu wa Israel ulianza tena vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza kwa mashambalizi ya anga dhidi ya eneo hilo.
Wizara ya Afya ya Gaza ilitangaza mwishoni mwa Ijumaa kwamba Wapalestina wasiopungua 178 wameuawa na 589 wamejeruhiwa tangu Israel kuanza tena kampeni yay a mauaji ya kimbari Gaza.
3486247