IQNA

Harakati za Qur'ani

Tarehe za Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani yatangazwa

11:47 - January 30, 2024
Habari ID: 3478276
IQNA - Maonesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yatafanyika wakati wa likizo ya Nowruz, yaani mwaka mpya wa Kiirani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani afisa mmoja alisema.

Ukumbi wa Sala (Mosalla) wa Imam Khomeini (RA) utakuwa mwenyeji wa hafla hiyo kuanzia Machi 20 hadi Aprili 3, Ali Reza Moaf, Naibu Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu ya Iran alisema.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari siku ya Jumatatu, alisema sikukuu za Nowruz itatoa fursa nzuri kwa watu kufaidika zaidi na maonyesho hayo.

Toleo hili la maonyesho litaandaliwa baada ya wiki mbili kwa njia nzuri na maarufu zaidi, Moaf alisema.

Ubora umetiliwa mkazo maalum katika sehemu tofauti za maonyesho, haswa sehemu ya watoto na vijana, mwaka huu, aliongeza.

Moaf amebainisha kuwa, nchi 25 hadi sasa zimeeleza utayarifu wao wa kushiriki katika tukio hilo la Qur'ani na kuongeza kuwa, suala la Palestina na muqawama wa watu wa Gaza, Lebanon, Yemen na Palestina ndilo litakalozingatiwa na sehemu ya kimataifa.

Afisa huyo aliendelea kusema kuwa maonyesho ya ndani ya Qur'ani pia yamepangwa kufanyika katika mikoa 30 ya nchi hiyo katika mwezi wa Ramadhani.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza dhana za Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani.

Inaonyesha mafanikio mapya zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

4196758

Habari zinazohusiana
captcha