IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Walemavu wa Macho yamalizika Tehran

16:13 - November 06, 2018
Habari ID: 3471731
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya walemavu wa macho yamemalizika Jumapili mjini Tehran kwa kuteuliwa wawakilishi wa Iran katika Awamu ya Nne ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Walemavu wa Macho.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika mashindano hayo kulikuwa na wasomaji (maqarii) 13 na waliohifadhi Qur'ani 17 kutoka mikoa 18 ya Iran.

 Jopo la majajai liliwatangaza Ahmad Dabbaq wa mkoawa Qom, Abdol Ghafour Joharchi kutoka mkoa Razavi Khroasan na Abdollah Mohammadnejad kutoka mkoa wa Sistan na Baluchestan kuwa wasomaji bora wa Qur'ani katika mashindano hayo kwa taratibu.

Katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu washindi  walikuwa ni Saeed Ali Akbari wa Qazvin, Omid Reza Rahimi wa Gilan na Saeed Hassanshahi wa  Fars kwa taratibu.

Wasita hao watashiriki katika mashindano mengine baina yao na mioni mwao wawili, qarii na hafidh, watachaguliwa kuiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano yajayo ya kimataifa.

Imedokezwa kuwa Awamu ya Nne ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Walemavu wa Macho imepangwa kufanyika mjini Tehran mwezi Mei mwaka 2019.

3761321

captcha