IQNA

Iran yamkumbuka malenga mkubwa Hafiz Shirazi

16:36 - October 11, 2020
Habari ID: 3473251
TEHRAN (IQNA)-Leo tarehe 20 mwezi wa Mehri kwa mujibu wa kalenda ya Kiirani, inasadifiana na maadhimisho ya Khaja Shamsuddin Muhammad Hafiz Shirazi, mshairi na malenga mkubwa wa Kiirani.

Hafiz alizaliwa mwaka 727 Hijiria Shamsia huko Shiraz moja ya miji ya kusini mwa Iran. Alikuwa mtaalamu katika tafsiri ya Qur'an, falsafa na fasihi ya Kiarabu na alipata umashuhuri kwa jina la Hafiz kutokana na kuhifadhi kwake Qur'an Tukufu kwa visomo tofauti. Mbali na elimu hizo, Khaja Shamsuddin Muhammad Hafiz, alikuwa mtaalamu mkubwa wa elimu ya Irfan. 

Mashairi ya Hafiz ambayo yanajulikana kama Ghazal kwa lugha ya Kifarsi yamefasiriwa kwa lugha kadhaa duniani. Kazi zake ziliwaathiri malenga maarufu akiwamo malenga maarufu wa karne ya 18 wa Ujerumani Johann Wolfgang von Goethe.

Ingawa jina lake kamili ni  Shamsuddin Mohammad, alipata umaarufu kwa lakabu yake ya Hafiz, kutokana na kuwa alikuwa amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu. Hafiz alitumi tafsiri ya Qur'ani kuwasilisha ujumbe wake kwa njia ya mashairi na hiyo kuwaletea watu utulivu katika nyoyo.

Picha zilizoko hapa chini ni za kaburi lake Hafiz Shirazi

3472793

 

captcha