IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Imani na izza ya taifa la Iran itapofua macho ya viongozi wahuni, watenda jinai wa Marekani

19:28 - October 12, 2020
Habari ID: 3473254
TEHRAN (IQNA)- Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, sababu ya makelele na bwabwaja za wahuni wapayukaji nchini Marekani kuhusiana na uwezo wa kiulinzi, makombora na kieneo wa Iran ni kwamba, wahusika wametambua mahesabu makini na ya kiakili ya taifa hili kwa ajili ya kufikia uwezo huu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo katika mahafali ya pamoja ya wahitimu wa vyuo vikuu vya kijeshi katika Chuo Kikuu cha Kijeshi  cha Imam Ali AS iliyofanyika kwa mawasiliano ya Intaneti na kueleza kwamba, bwabwaja na upayukaji wa Wamarekani unatokana na woga na kubakia kwao nyuma katika uga huu. 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, vyombo husika vya mahesabu ya kiakili vinapaswa kupuuza propaganda hizo na kufanya mambo yao na bila shaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kupiga hatua pia katika nyuga zote hizi.

Ayatullah Khamenei ameashiria hatua ya Rais wa Marekani ya kufurahishwa na dosari katika uchumi wa Iran na jinai dhidi ya wananchi wa taifa hili na kubainisha kwamba, kujifakharisha na jinai kama hizi ni jambo linaloweza kufanywa na watu wahuni kama wewe.

Amiri Jeshi Mkuu  wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hii leo hali ya Marekani ni mbaya mno ambapo nchi hiyo inakabiliwa na nakisi ya bajeti ya mabilioni ya dola huku kukiwa na makumi ya mamilioni ya watu wanaotaabika kwa njaa nchini humo.

Aidha amesema, taifa la Iran likiwa na nguvu ya imani na izza ya kitaifa litapofua macho ya viongozi wahuni, wasaliti na watenda jinai wa Marekani kwa kuyashinda matatizo yote na watatumia vikwazo kama wenzo wa kuimarisha uchumi wa taifa lao.

/3928754

captcha