Katika klipu hii ya hivi karibuni, Sheikh Shahat anasikika akisoma aya za 2 na 3 za Surah Al-Hadid zisemazo: " Yeye ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha. Na Yeye ni Mwenye uweza wa kila kitu. Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhaahiri na wa Siri, naye ndiye Mjuzi wa kila kitu."
Al-Hadidi ni Surah ya 57 ya Qur'ani Tukufu na ina aya 29. Al-Hadid maana yake ni chuma na neno hilo limetumika katika aya ya 25 ya Surah hiyo.