IQNA

Mtaalamu wa Kuwait: Kuanzisha uhusiano na Israel ni ukoloni mamboleo

16:48 - October 13, 2020
Habari ID: 3473257
TEHRAN (IQNA) – Mtaalamu maarufu wa kisiasa Kuwaita amelaani hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia na Israel na kutaja hatua hiyo kuwa sawa na ukoloni mamboleo.

Abdullah al-Nefisi ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, kutiwa saiani mapatano  ya uhusiano wa kidilomasia baina ya Israel na nchi za Kiarabu kutazifanya nchi hizo za Kiarabu kuwa koloni mpya.

"Uhusiano wa kawaida na utawala wa Israel ni ukoloni mamboleo kwani utabadilisha nchi zetu kuwa koloni zenye kuhudumia maslahi ya pamoja ya Marekani na Wazayuni."

Amiri mpya wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad al Jaber al Sabah amesema nchi yake itaunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina. Katika mkutano na Waziri Mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh, Sheikh Nawaf alisema atafuata nyayo za marehemu Amiri wa Kuwait  Sheikh Sabah al-Ahmad al-Jaber Al Sabah ambaye alikuwa muungaji mkono wa Palestina.

Amir wa Kuwait, Sheikh Sabah al-Ahmad al-Jaber al-Sabah aliaga dunia huko nchini Marekani tarehe 29 ya mwezi uliopita wa Septemba akiwa na umri wa miaka 91 baada ya kuugua.

Wakati wa uhai wake Sheikh al-Sabah alifahamika zaidi kama mbunifu wa sera za nje za enzi hizi nchini Kuwait na pia msuluhishi na mpenda amani.

Kuwait imekuwa ikisitiza mara kwa mara juu ya msimamo wake thabiti na usiotetereka kuhusiana na kadhia ya Palestina pamoja na haki za wananchi hao madhulumu huku ikiunga mkono kuundwa nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa Baitul-Muqaddas.

Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain baada ya kufikia mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel unaoikalia Quds kwa mabavu; tarehe 15 mwezi Septemba mwaka huu zilisaini huko White mapatano ya kuanzisha uhusiano rasmi na utawala huo wa Kizayuni. Tukio hilo lilihudhuriwa na Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

3472811

captcha