IQNA

Saudia yashindwa kuijiunga na Baraza la Haki za Binadamu la UN

10:52 - October 14, 2020
Habari ID: 3473258
TEHRAN (IQNA) – Saudi Arabia imeshindwa kujiunga na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kufuatia pingamizi la shirika moja la kimataifa.

Katika upigaji kura uliofanyika siku ya Jumanne Saudia ilipata kura 90 kati ya kura 193 wakati wa upigaji kura wa kujiunga na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Saudia imefeli katika mpango wake huo baada ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kupinga hatua hiyo ya Saudia.

Human Rights Watch imeituhumu Saudia kwa kukiuka haki za binadamu a kuwakandamiza watetezi wa haki za binadamu na wapinzani wa kisiasa. Shirika hilo limesema Saudia hukiuka haki za binadamu mara kwa mara. Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa watoto 7,200 wameuawa au kujeruhiwa katika hujuma ya Saudia dhidi ya Yemen tokea mwaka 2015.

Louis Charbonneau mkurugenzi wa Human Rights Watch amesema wakiukaji wa haki hawapaswa kutunukiwa viti katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Machi 2015 Saudi Arabia, ikiungwa mkono na  Marekani, Imarati na nchi zingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen na kuiwekea mzingiro wa kila upande nchi hiyo. Moto wa vita uliowashwa na Saudia na waitifaki wake nchini Yemen hadi sasa umesha sababisha makumi ya maelfu ya watu kuuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.

Uvamizi wa kijeshi wa Saudia umeisababishia pia nchi masikini ya Yemen uhaba mkubwa wa chakula na dawa.

3472825

captcha