IQNA

Waziri Mkuu wa Canada asema hataruhusu chuki dhidi ya Uislamu nchini humo

20:38 - October 14, 2020
Habari ID: 3473260
TEHRAN (IQNA) – Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) pamoja na misimamo mikali ya mrengo ya kulia ni itikadi ambazo hazina nafasi yoyote katika jamii ya Canada.

Trudeau ametoa kauli hiyo baada ya msikiti mmoja mjini Toronto kupokea vitisho. Amesema amekerwa sana baada ya msikiti mmoja mjini Toronto kupokea tishio la kushambuliwa. Waliotoa tishio wameashiria hujuma ya kigaidi iliyolenga msikiti mjini New Zealand mjini Christchurch ambapo Waislamu zaidi ya 50 waliuawa wakati wa swala ya Ijumaa mwaka jana.  Waziri Mkuu wa Canada amesema atachukua hatua zaidi za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu.

Siku chache zilizopita msikiti mmoja mjini Toronto ulipokea baruapepe iliyosema:  “Tuko na bunduki za kutekeleza hujuma sawa na iliyojiri Christchurch.”

Msikiti huo haukutajwa kwa sababu za kiusalama huku polisi wakisema wanafanya uchunguzi kuhusu tishio hilo. Kundi la wabunge Waislamu nchini Canada wamebainisha wasiwasi wao kuhusiana na ongezeko la ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya Uislamu na itikadi kuwa wazungu ndio wanadamu bora kuliko wengine wote.

3472834

captcha