IQNA

Israel yajenga vitongoji vipya hata baada ya kuanzisha uhusiano na Waarabu

21:30 - October 15, 2020
Habari ID: 3473263
TEHRAN (IQNA) – Utawala wa Kizayuni wa Israel umeidhinisha ujenzi wa nyumba mpya 2,166 za walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Uamuzi huo umekuja chini ya mwezi mmoja baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain kusiani mapatano ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel. Nchi hizo mbili za Kiarabu zilikuwa zimedai kuwa moja ya masharti ya mapatano hayo ni Israel kusitisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi.

Mapema mwezi huu, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilipinga madai ya afisa mwandamizi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuwa eti utawala bandia wa Israel umesitisha upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni baada ya utawala huo kuanzisha uhusiano na nchi mbili za Kiarabu za UAE na Bahrain.

Msemaji wa Hamas Hazem Qasim alitoa taarifa na kusema upanuzi usio na kikomo wa vitongozji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukiongo wa Magharibi ni jambo ambalo limeweka wazi madai yasiyo na msingi ya tawala za Kiarabu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE Sheikh Abdullah bin Zayed bin Sultan Al Nahyan amedai kuwa mapatano ya nchi yake na Israel yameulazimu utawala huo bandia kusitisha upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.

Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain baada ya kufikia mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel unaoikalia Quds kwa mabavu; tarehe 15 mwezi Septemba mwaka huu zilisaini huko White mapatano ya kuanzisha uhusiano rasmi na utawala huo wa Kizayuni. Tukio hilo lilihudhuriwa na Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

3472838

captcha