IQNA

Misri yaizawadia Mauritius nakala za Qur’ani Tukufu

19:54 - October 16, 2020
Habari ID: 3473264
TEHRAN (IQNA) – Balozi wa Misri nchini Mauritius amewatunuku wakuu wa jumuiya mbali mbali za Kiislamu Mauritius nakala za Qur’ani ambazo zina tarjama ya lugha mbali mbali.

Balozi Bi. Aya Saeed amewatunuku wakuu wa  jumuiya za  ‘Hila Al Arzaq’, na ‘Baitul Qur’an’ nakala kadhaa za Qur’ani Tukufu.

Balozi huyo ameelezea matumaini yake kuwa nakala hizo za Qur’ani zitaweza kutumika kueneza mafundisho sahihi ya Kiislamu na kukabiliana na watu wenye kupotosha dini na wenye misimamo mikali ya kufurutu ada.

Jamhuri ya Mauritius (Morisi) ni kisiwa kilicho katika Bahari ya Hindi yapata kilomita 2,000 kusini mashariki mwa pwani ya Afrika.

Waislamu ni asilimia 20 ya watu wote wa Malayasia. Waislamu wa Mauritisu ni wenye asili ya India lakini kuna idadi kubwa waliosilimu kutoka kaumu ya Creole.

3929526

captcha