IQNA

Siku ya Maulid ya Mtume Muhammad SAW iwe ‘Siku ya Kimataifa ya Rehema’

20:04 - October 16, 2020
Habari ID: 3473266
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Pakistan wamependekeza kuwa siku ya kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad SAW, ambayo ni maarufu kama Maulid, iadhmishwe pia kama ‘Siku ya Kimataifa ya Rehema”.

Pendekezo hilo limewasilisha na Syed Abdullah Tarek na wengine na wanasema wana matumaini kuwa siku kama hiyo itatumika kurekebisha taswira potovu iliyopi kuhusu Uislamu na ufahamu usio sahihi walionao  wengi wasiokuwa Waislamu kumhusu Mtume Muhammad- Rehema na Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu Yake na Familia Yake- (SAW).

Wamesema  katika ‘Siku ya Kimataifa ya Rehema’, watu wote watatakiwa kutekeleza vitendo vya huruma, kuhurumiana na mapenzi kwa wanadamu wengine.

Waliotoa pendekezo hilo pia wanatumai kuwa siku kama hiyo itakuwa ni msukumo kwa Waislamu kuimarisha mapenzi na mahaba yao kwa Mtume wa Rehema.

Mwenyezi Mungu SWT katika  Qur’ani Tukufu Sura ya Al Anbiya aya ya 107 anasema: “Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.”

Maulid ya Mtume Muhammad SAW ambayo itaanza kuadhimishwa mwezi wa Rabiul Awwal unaotazamiwa kuanza Jumapili Oktoba 19 ni mwezi ambao Waislamu kote duniani hukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad SAW.

3929610

captcha