IQNA

Uchaguzi wa rais Marekani 2020

Biden asema atawateuea Waislamu katika ngazi zote za serikali yake

13:59 - October 17, 2020
Habari ID: 3473269
TEHRAN (IQNA) – Mgombea kiti cha urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden amesema atawateua Waislamu nchini humo katika ngazi zote za kijamii na kisiasa za serikali yake endapo atashinda katika uchaguzi.

Katika ujumbe kwa njia ya video siku ya Jumatano, Biden amesema  katika siku ya kwanza baada ya kuapishwa, ataondoa ‘marufuku ya Waislamu’ ambayo inatekelezwa na rais Donald Trump.  Biden aidha amesema atawashinikiza wabunge wapitishe sheria ya kukabiliana na ongezeko la jinai za chuku nchini Marekani.

Kauli hiyo ya Biden ni ya pili kwa Waislamu tokea ateuliwa kupeperusha bendera ya Wademocrat katika uchaguzi wa rais utakaofanyika Novemba 4.

Pamoja na kuwa Waislamu ni jamii ndoge ya wapiga kura Marekani lakini wako katika majimbo muhimu ambayo Trump alipata ushindi mdogo sana mwaka 2016, likiwemo jimbo la Michigan. Ni kwa msingi huo ndio Wademocrat wanataka kuwashawishi Waislamu wajitokeze kwa wingi ili kumuangusha Trump.

Mbunge Muislamu Rashida Tlaib ametoa wito kwa Waislamu kujitokeza kwa wingi ili kumuangusha Trump ambayo ametangaza marufuku ya Waislamu kuingia nchini humo.

3929438

captcha