IQNA

Klipu nadra ya Sheikh Abdul Basit akisoma aya za Surah Fussilat

11:40 - October 19, 2020
Habari ID: 3473274
TEHRAN (IQNA) – Klipu nadra ya video imesambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha qarii mashuhuri wa Misri marhum Sheikh Abdul Basit Abdul Samad akisema aya za Surah Fussilat.

Klipu hiyo inamuonyesha qarii huyo akisema aya za 30 hadi 33 za Surah Fussilat katika Qur'ani Tukufu.

"Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyo kuwa mkiahidiwa.  mtapata kinacho tamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyo vitaka. Ni takrima itokayo kwa Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.   Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?"

Abdul Basit alizaliwa mwaka 1927 katika kijiji cha Almazaizah katika eneo la Armant kusini mwa Misri. Sheikh Abdul Basit Abdul Swamad alikamilisha hifdhi ya Qur'ani akiwa na umri wa miaka 10 kijijini kwake kwa Ustadh Al Amir na akahitimu aina zote za kiraa ya Qur'ani akiwa na umri wa miaka 14.

Abdul Basit alipewa lakabu ya 'Koo ya Dhahabu' kutokana na kiraa yake ya kuvutia na alipendwa mno na wafuatiliaji wa masuala ya Qur'ani kwa kadiri kwamba hadi sasa anatambuliwa kuwa qarii mashuhuri na anayepesndwa zaidi wa Qur'ani.

Qari huyo mashuhuri wa Misri aliaga dunia tarehe 30 Novemba mwaka 1988 katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

Qiraa ifuatayo  ni ya mwaka 1980 katika msikiti wa Al Rifa'i mjini Cairo.

3929765

captcha