IQNA

Marekani kufunga tovuti za vyombo vya habari ni ukiukwaji uhuru wa maoni

22:08 - June 29, 2021
Habari ID: 3474053
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Redio na Televisheni za Kiislamu amehutubu amsema hatua ya Marekani kufunga tovuti kadhaa za televisheni wanachama wa jumuiya hiyo ni ukiukaji wa wazi wa uhuru wa maoni.

Hujjatul Islam Mohammad Ali Karimian Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wa Redio na Televisheni za Kiislamu ameyasema hayo leo katika kikao cha 10 cha jumuiya hiyo ambacho kimeitishwa kujadili ‘Uadilifu wa Vyombo vya Habari na Uhuru wa Kusema." Amesema kutokana na janga la corona baraza kuu la jumuiya hiyo haltakuwa na mkutano mwaka huu.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Idhaa na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) ameashiria ukwamishaji wa ubeberu wa kimataifa na Uzayuni chini ya uongozi wa Marekani katika kukabiliana na vyombo vya habari vya muqawama na kueleza kuwa vyombo hivyo vitaendeleza njia yake kwa nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma.

Abdulali Ali Asghari ameongeza kuwa vyombo hivi vinaungwa mkono na watu wenye dhamira ya dhati, wanajihadi na jasiri na kwamba vitaendeleza njia yake hiyo. Ali Asghari amesisitiza kuwa kwa kufunga vyombo hivyo vya muqawama maaadui hawatopata faida yoyote na kwamba watambue kuwa katika siku zijazo vyombo vya habari vya muqawama vitakuwa na nguvu kubwa zaidi kuliko huko nyuma; na ukitupia jicho utaliona hili na Mwenyezi mungu ameahidi ushindi. 

Mkutano huo umehuhudhuriwa na wawakilishi wa vyombo vya habari kutoka nchi mbalimbali ambao wameshiriki kwa njia ya intaneti.

Wiki iliyopita, serikali mpya ya Marekani iliendeleza sera za kiijuba ya kibeberu za nchi hiyo kwa kuzifunga tovuti za televisheni za kimataifa za Iran na vyombo vya habari vya mrengo wa muqawama au mapambano ya Kiislamu Yemen, Palestina, Iraq na Bahrain.

Televisheni ya Kiingereza ya Iran ya Press TV na zile za Kiarabu za Al Alam na Al Khauthar ni kati ya vyombo vya habari ambavyo vimefunguiwa tovuti zao na Marekani.

Kufuatia hatua hiyo Press TV imetangaza kuwa tovuti iliyofungwa ya presstv.com  sasa inapatikana kupitia presstv.ir

3980928

captcha