IQNA

Uchaguzi wa 'bunge' wafanyika kwa mara ya kwanza Qatar

22:50 - October 03, 2021
Habari ID: 3474377
TEHRAN (IQNA)- Kwa mara ya kwanza, raia wa Qatar wamepiga kura Jumamosi Oktoba 3 katika uchaguzi wa bunge, ikiwa ni ishara ya kuendelea marekebisho ya kisiasa kwa lengo la kuwashirikisha wananchi katika utawala atika taifa hilo dogo lenye utajiri wa mafuta katika Ghuba ya Uajemi..

Wapigakura waliingia vituoni wakitenganishwa wanawake na wanaume mbali, kuwachaguwa wajumbe 30 kati ya 45 wa bunge hilo liitwalo Baraza la Shuraa, ambapo nafasi 15 zilizosalia zitajwa kwa uteuzi utakaofanywa na kiongozi wa taifa hilo, afahamikaye kama amiri. 

Baraza la Shuraa litakuwa na mamlaka ya kibunge, yakiwemo ya kuidhinisha sera kuu za taifa na bajeti.

Hata hivyo, Baraza la Shuraa halitakuwa na mamlaka juu ya  baraza la mawaziri, ambalo ndilo linalotunga sera za ulinzi, usalama, uchumi na uwekezaji kwa taifa hilo dogo na tajiri kwa uzalishaji wa mafuta, ambalo limepiga marufuku vyama vya kisiasa.

Orodha iliyotolewa na serikali inaonesha kuwa katika wagombea 234 waliowania uwakilishi wa wilaya 30 za nchi hiyo, 26 ni wanawake.  Kwa mujibu wa taarifa, asilimia 63.5 ya waliotimiza masharti ya kupiga kura walijitokeza katika uchaguzi huo.

Kwa muda mrefu, Qatar imekuwa ikifanya chaguzi za mabaraza ya miji, lakini uchaguzi wa huu wa bunge ni wa kwanza na wa aina yake, ambapo wagombea walijinadi kupitia mitandao ya kijamii, mikutano ya hadhara na mabango ya barabarani. 

Uchaguzi huu, ambao ulipitishwa kwenye kura ya maoni ya katiba ya mwaka 2003, unafanyika wakati Qatar ikijiandaa kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka ujao.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani, mwezi jana alisema uchaguzi huu wa baraza hilo ni ‘jaribio’ jipya na kuongeza kuwa haliwezi kuwa na ya bunge katika duru hii ya kwanza.

3475888

 

Kishikizo: qatar uchaguzi
captcha