IQNA

Maonyesho makubwa zaidi ya Imam Ali AS barani Ulaya yanafanyika London + Video

16:59 - October 11, 2021
Habari ID: 3474412
TEHRAN (IQNA)- Mji mkuu wa Uingereza, London, hivi sasa ni mwenyeji wa maonyesho makubwa na ghali zaidi ya Kiislamu ambayo yanaangazia kikamilifu maisha ya binamu yake Mtume Muhammad SAW, Imam Ali AS.

Maonyesho hayo yanampelekea mtazamaji katika safari kuhusu maisha ya Ali ibn Abi Talib ambaye utumishi na utiifu wake ulikuwa na mchango mkubwa na wa kudumu katika Uislamu.

Imam Ali AS ni kipenzi cha Waislamu wote na hata wasiokuwa Waislamu dunaini. Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanamtazama kama Khalifa wa Nne aliyeongoka nao Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaamini kuwa yeye ndiye Imamu wa kwanza kati ya Maimamu 12 watoharifu kutoka Kizazi cha Mtume Muhammad SAW.

Naye msomi Mkristo, George Jordac wa Lebanon ameandika kuhusu adhama ya Imam Ali AS katika kitabu chenye chini ya anuani ya 'Sauti ya Uadilifu wa Binadamu".

Maonyesho hayo yanaipa jamii fursa ya kuangazia mmoja kati ya viongozi muhimu zaidi wa Kiislamu na kujifunza mapya kuhusu maisha yake.

Kundi la The Legacy ambalo limeandaa maonyesho hayo linasema linalenga kuangazia kikamilifu maisha ya Imam Ali AS ili Waislamu waweze kuhisi ufungamano halisi na shakhsia huyu mkubwa wa Kiislamu.

Mmoja kati ya wasimamizi wa maonyesho hayo, Hasanain Baraka anasema kimsingi waliamua kuandaa maonyesho ya Imam Ali AS kwa sababu watoto wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu famili ya Mtume Muhammad SAW na waliosikia husahau. Anasema maonyesho kama haya, kinyume na vitabu, yanaweza kuacha taathira kubwa katika fikra za wanaoyatembelea na kuhisi kana kwamba wako katika zama za tukio.

3475994/

captcha