IQNA

Waislamu wa Thailand

Thailand yamteua gavana wa kwanza mwanamke Mwislamu

16:56 - November 17, 2022
Habari ID: 3476104
TEHRAN (IQNA) - Thailand imemteua gavana wa kwanza mwanamke Mwislamu katika jimbo la kusini la Pattani katika kitendo ambacho waangalizi wanaamini kinaweza kusaidia kumaliza migogoro.

Pateemoh Sadeeyamu, 57, ameteuliwa kuwa gavana mpya wa jimbo la Pattani kusini.

Baraza la Mawaziri la Thailand liliidhinisha uteuzi Jumanne.

Akiwa na uzoefu wa takriban miaka 29 katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya taifa hilo lenye Wabuddha wengi, awali aliwahi kuwa naibu gavana wa jimbo la Narathiwat.

“Haya ni maendeleo makubwa. Kuwa Mwislamu na mwanamke kuna changamoto nyingi katika siasa za Thailand,” Yasmin Sattar, makamu mkuu wa Masomo, Utafiti na Mambo ya Nje katika Chuo Kikuu cha Prince of Songkla, Pattani, amesema.

"Tumeweza kuona kuboreka kwa wanawake wa Kiislamu katika siasa," Sattar alisema kuhusu Sadeeyamu.

Kati ya majimbo 77, majimbo manne ya kusini ya Pattani, Yala, Narathiwat, na Songkla yameshuhudia mizozo kwa miongo kadhaa huku National Revolution Front likiwa kundi kuu la waasi waliokuwa wanapigana kujitenge eneo hilo lenye Waislamu wengi.

Kuinuliwa kwa Sadeeyamu kama gavana wa mkoa kunaonekana kama " hatua ya italayoleta mtazamo mzuri miongoni mwa Waislamu waliowengi eneo hilo."

Hii inaweza kuinua Imani ya Waislamu waliowengi katika eneo hilo la Thailand na ni hatua muhimu katika kumaliza mzozo uliopo, alisema Sattar kuhusu juhudi za amani kati ya serikali ya Thailand na makundi ya waasi katika mikoa ya kusini.

Uasi kusini mwa Thailand ulianza mnamo 1948 kama mzozo wa kikabila na kidini katika eneo la kihistoria la Malay Patani.

Mikoa ya Pattani Kusini, Yala, Narathiwat, na Songkhla ina jumuiya kubwa ya Wamalay-Waislamu - Patani - yenye wakazi milioni 1.4, kulingana na data ya serikali.

Serikali ya Thailand iliweka sheria ya kijeshi katika majimbo matatu yenye Waislamu wengi kusini mwa Thailand - Pattani, Narathiwat, na Yala - kufuatia ghasia mbaya mwaka 2004.

Kulingana na kundi la ufuatiliaji la Deep South Watch, zaidi ya watu 7,000 waliuawa na 13,000 kujeruhiwa katika uasi ulioanza mwaka 2004 na kumalizika  mwaka 2020.

3481289

captcha