IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Misri kuzindua Mashindano ya walimu wa Qur'ani

18:50 - November 29, 2022
Habari ID: 3476170
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Wakfu ya Misri imesema inazindua mashindano ya walimu wa Qur'ani nchini humo.

Wizara hiyo ilisema mashindano hayo, ambayo yataanza Jumanne, yanalenga kuimarisha ujuzi na umahiri wa Qur'ani kwa walimu.

Taarifa hiyo ilisema mashindano ya Qur'ani pia yatasaidia kukuza umakini wa kuhifadhi na kusoma Qur'ani na kuelewa maana, dhana na malengo matukufu ya Kitabu hicho Kitukufu.

Msikiti wa Al-Rahma mjini Cairo na misikiti katika majimbo mengine matano ya Misri ndio utakaoandaa mashindano hayo, kwa mujibu wa wizara hiyo.

Pia imesema katika taarifa yake kwamba duru za Qur'ani zitaendelea kufanyika katika majimbo tofauti ikiwemo Gharbia, Sharqia, Alexandria, Cairo na Monufia.

Programu hizo hupangwa misikitini baada ya sala ya Alasiri na ni pamoja na usomaji wa Qur'ani Tukufu na hotuba zinazojumuisha sayansi za Qur'ani.

Zinakusudiwa kukuza umakini wa Qur'ani Tukufu na pia kuinua kiwango cha wanawake katika jamii, wizara iliendelea kusema.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Kurani ni za kawaida sana katika nchi ya Kiarabu na wengi wa qari wakuu wa ulimwengu wa Kiislamu hapo zamani na sasa wamekuwa Wamisri.

4102955

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu misri
captcha