IQNA

Kongamano la Kimataifa mjini Tehran lajadili urithi wa Ayatullah Mesbah Yazdi

TEHRAN (IQNA) - Kongamano la kimataifa limefanyika hapa Tehran Jumamosi kwa heshima ya marehemu mwanazuoni mashuhuri Ayatullah Mesbah Yazdi. Kongamano hilo ambalo lilihutubiwa na Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran liliandaliwa katika kumbukumbu ya pili ya kifo cha mwanazuoni huyo chini ya kaulimbiu ya 'Mwalimu wa Mawazo'.