IQNA

Kongamano la Kimataifa la 'Fikra za Shahidi Soleimani' lafanyika Tehran

TEHRAN (IQNA) – Kongamano la Kwanza la Kimataifa la 'Fikra za Shahidi Soleimani' lilizinduliwa katika hafla iliyofanyika mjini Tehran siku ya Jumatano.

Kongamano hilo la siku mbili limehudhuriwa na wanazuoni, shakhsia wa kisiasa na maafisa wa muqawama kutoka nchi mbalimbali na limeandaliwa katika mwaka wa tatu tokea auawe shahidi kamanda huyo mkubwa wa Iran.