IQNA

Wanasoka Waislamu

Tizama mchezaji wa zamani wa Arsenal akisoma Qur'ani Tukufua +Video

TEHRAN (IQNA)-Klipu ya video inaendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii ikumuonyesha mchezaji wa zamani wa Timu ya Soka ya Arsenal ya Uingereza, Vassiriki Abou Diaby akisoma aya za Qur'ani Tukufu.

Klipu hiyo inamuonyesha Abou Diaby, ambaye pia aliwahi mkuwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Soka ya Ufaransa, akisoma Qur'ani kwa mbinu ya Tartil.

Inaaminika kuwa klipu hiyo ya video inahusiana na msimu wa Hija wa mwaka 1438 Hijria Qamaria katika moja ya maheama ya eneo la Mina.

Abou Diaby alipata umaarufu kama mchezaji wa Ligi ya Premier ya England ambaye alikuwa amehifadhi Juzuu 19 za Qur'ani Tukufu. Tizama kilipu ya video hapo chini.

Hii hapa klipu ya Abou Diaby  akisoma aya ya 1 hadi 14 katika Sura Taha kwa kuzingatia kanuni za usomaji Qur'ani.

T'AHA! 

Hatukukuteremshia Qur'ani ili upate mashaka. 

Bali ni mawaidha kwa wenye kunyenyekea.

Materemsho yatokayo kwa aliye umba ardhi na mbingu zilizo juu. 

Arrahmani, Mwingi wa Rehema, aliye tawala juu ya Kiti cha Enzi. 

Ni vyake vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na viliomo baina yao, na viliomo chini ya ardhi. 

Na ukinyanyua sauti kwa kusema...basi hakika Yeye anajua siri na duni kuliko siri. 

Mwenyezi Mungu! Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Yeye ana majina mazuri kabisa. 

Na je! Imekufikia hadithi ya Musa?

Alipo uona moto, akawaambia watu wake: Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikakuleteeni kijinga kutoka huo moto, au nikapata uongofu kwenye moto. 

Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe Musa! 

Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa. 

Nami nimekuteua wewe; basi sikiliza unayo funuliwa. 

Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi. 

4112763

Kishikizo: abou diaby ، arsenal ، qurani tukufu