IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu /18

Mustafa Mahmoud; Mwanachuoni aliyefikia uhakika baada ya shaka

17:33 - January 27, 2023
Habari ID: 3476472
TEHRAN (IQNA) - Mustafa Mahmoud alikuwa mtafiti wa Qur'ani Tukufu nchini Misri, aidha aliluwa daktari, mtunzi wa fasihi na mtayarishaji wa vipindi vya televisheni.

Kwa muda wa  zaidi ya miongo mitano aljitahidi sana kutoa miongozo ya ufahamu sahihi sayansi kwa mujibu wa Uislamu huku pia akitoa mafunzo kuhusu  imani na maadili katika zama za kisasa.

Mustafa Kamal Mahmoud Hussein Al Mahfouz (Desemba  27, 1921  - Oktoba 31, 2009) aliandika vitabu 89 katika nyanja za tafsiri ya Qur'ani, mawazo ya kidini, riwaya, tamthilia na simulizi za safari.

Kwa kuzingatia mazingira ya kiakili ya wakati huo, Mahmoud, ambaye alisomea udaktari, aliuchukulia ulimwengu wa kimaada (material world) kuwa wenye kuainisha hatima na aliamini kuwa mwanadamu hana hiari katika ulimwengu huu.

Hata hivyo, baada ya miaka mingi ya kutafakari na masomo, alikuja kuamini kwamba uwepo wa ulimengu wa kimaada hauwezi kuwa unaishia hapo bali maamuzi huru ya mwanadamu yanatokana na dhati yake binafsi. Aliandika kitabu kuhusu safari yake kutoka kwa shaka hadi uhakika kuhusu imani ya Kiislamu. Katika hitabu hicho  kilichochapishwa mnamo 1970, anakosoa hadhi ya Qur'an katika jamii ya Misri wakati huo na kusema ukweli kwamba muujiza wa Qur'ani Tukufu umebaki umefichwa ni kwa sababu ya ufahamu usio sahihi na mbinu ya kukisoma Kitabu hicho Kitukufu.

Aliamini kwamba wasomaji (maqari) wakati huo walisoma Qur'ani Tukufu bila kuzingatia maana ya aya, na mbinu hii haikuwasaidia wasikilizaji kuelewa dhana za aya.

Katika kitabu kingine kiitwacho “Mungu na Mwanadamu”, Mahmoud alijaribu kujibu maswali ya kimsingi kuhusu shaka, yakini, tauhidi na Kufr (kutokuamini). Wengi waliona kitabu hicho kuwa cha kufuru. Lakini kikao cha mahakama kilichoendeshwa kwa ombi la rais wa wakati huo wa Misri Gamal Abdel Nasser kilimuondolea mashtaka ya lugha chafu.

Rais mwingine, Anwar Sadat, ambaye alikuwa rafiki wa Mahmoud, alimwomba achapishe kitabu hicho chini ya jina la "Mazungumzo Yangu na Rafiki Yangu asiyeamini Mungu".

Baadaye, Mahmoud alitoa uhakiki wa maoni aliyoyatoa katika kitabu hiki, akiyaelezea kama jukwaa kwenye njia yake kutoka kwa shaka hadi yakini.

Mojawapo ya kazi zake bora ilikuwa kipindi cha televisheni kilichoitwa "Sayansi na Imani", ambacho kilionyeshwa kwenye TV ya Misri kwa miaka 28 (kutoka 1971 hadi 1999) katika vipindi 400.

Kipindi hiki kIliangazia mijadala juu ya sayansi yenye msingi wa imani. Katika kipindi hicho, angezungumza kwanza kuhusu maendeleo ya kisayansi katika ulimwengu wa kisasa na kisha kutaja aya za Qur'an na tafsiri yake ili kujadili mambo yenye mafunzo kama vile haja ya kukimbilia imani ili kujilinda kutokana na utumiaji vibaya wa sayansi.

captcha