IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu Marekani

Ilhan Omar: Warepublican hawataki kuona Wabunge Waislamu katika Kongresi ya Marekani

17:28 - February 01, 2023
Habari ID: 3476497
TEHRAN (IQNA)- Ilhan Omar, Mbunge Mwislamu wa chama cha Democratic katika Baraza la Wawakilishi la Marekani anayewakilisha jimbo la Minnesota amesema kuwa, baadhi ya wajumbe wa chama cha Republican hawataki kuona kunakuweko na Wabunge Waislamu katika Kongresi ya nchi hiyo.

Amesema, ndio maana kumekuwa kukifanyika kampeni na njama za kuwakwamisha kwani wanataka watu wenye chuki dhidi ya Uislamu ndio waingie katika Bunge la nchi hiyo.

Kuhusiana na juhudi za Kevin McCarthy Mbunge wa jimbo la California ambaye pia ni Spika wa Bunge la Marekani za kutaka kumuondoa katika Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Bunge hilo, Bi Ilhan Omar mwenye asili ya Somalia amesema, baadhi ya wajumbe wa chama cha Republican wanaafikiana na kampeni chafu za chuki dhidi ya Uislamu.

Mbunge huyo wa Kiislamu katika Kongresi ya Marekani ameongeza kuwa, wanachama wa chama cha Republican kama Kevin McCarthy hawakubaliani kabisa la suala la kuweko Mbunge Mwislamu katika Kongresi ya Marekani ambaye atakuwa ni sauti ya Waislamu wengine.

Kadhalika amesema, akthari ya wajumbe wa chama chah Republican wanaamini kuwa, Mwislamu, mhajiri na Muafrika hapaswi kabisa kuwa mwakilishi katika Bunge la Marekani seuze awepo katika Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Bunge la nchi hiyo.

Suala la chuki dhidi ya Uislamu na kampeni za kueneza chuki dhidi ya Uislamu na kukabiliana na Waislamu sambamba na kuwakwamisha wasishike nyadhifa nyeti nchini Marekani hususan zile zinazoendeshwa na wanachama wa chama cha Repulican wenye misimamo ya kufurutu ada dhidi ya Waislamu ni hatua ambazo zimechukua wigo mpana zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

3482283

captcha