IQNA

Alfajiri 10 za Mapinduzi ya Kiislamu

Wananchi wa Iran waanza kusherehekea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

17:44 - February 01, 2023
Habari ID: 3476499
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Iran wameanza sherehe za Alfajiri Kumi katika kona zote za nchi kwa ajili ya kuadhimisha miaka 44 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 nchini Iran ambayo yaliupindua utawala wa kitaghuti wa Kipahlavi uliokuwa unaungwa mkono kila upande na Marekani.

Sherehe hizo zimeanza rasmi leo Jumatano asubuhi kwa saa za hapa Iran. Sherehe kama hizo zimefanyika pia kote nchini Iran ikiwa ni pamoja na kudondoshwa maua juu ya Haram ya Imam Khomeini, Mwenyezi Mungu amrehemu kama njia ya kukumbuka siku mwasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliporejea nchini kutokea Ufaransa alikokuwa amepelekwa kwa nguvu na utawala wa kifalme wa wakati huo.

Miaka 44 iliyopita katika siku kama ya kesho ya leo 12 Bahman 1357 Hijria Shamsia (tarehe 1 Februari 1979), Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alirejea nchini na kulakiwa kwa shauku kubwa na umati mkubwa wa watu na kukanyaga tena ardhi ya Iran ya Kiislamu baada ya kuwa mbali na nchi yake na kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka 15.

Siku kumi baada ya Imam Khomeini kuwasili Iran, yaani tarehe 22 Bahman 1357 (Februari 11, 1979), Mapinduzi matukufu ya Kiislamu ya Iran yalipata ushindi kamili.
Kwa sababu hiyo, kuanzia tarehe 12 Bahman, siku ambayo Imam Khomeini (MA) aliwasili nchini, hadi tarehe 22 Bahman, ambayo ni siku ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, imepewa jina la Alfajiri Kumi, ambapo kila mwaka hufanyika sherehe na hafla maalumu katika masiku hayo kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu..

Wakati huo huo, Spika wa Bunge la Iran Mohamma Bagher Qalibaf Jumatano alishiriki katika Sherehe za kukumbuku siku aliporejea Imam Khomeini nchini Iran Februari 1, 1979, na kuongoza moja kwa moja Mapinduzi ya Kiislamu. Akihutubia wananchi katika Haram ya Imam Khomeini MA, Qalibaf amesema: "Imam Khomeini (MA) ni Mja wa Mwenyezi Mungu ambaye aliibukia kutoka katika vyuo vya Kiislamu katika zama za kudhulumiwa dini iwe ni katika ulimwengu wa Kiislamu au maeneo mengine duniani na katika zama ambazo Wakomunisti wa  mabeberu wa Magharibi walikuwa wameeneza satwa yao duniani kote. Kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na kisha kwa kuwategemea wananchi azizi wa Iran ya Kiislamu na kwa Imani imara alianzisha harakati ya mwamko na hatimaye kuondoa Uislamu katika hali ya kutengwa. Aliweza kuliokoa taifa la Iran kutoka katika makucha ya udikteta. Imam pia aliweza kueneza moyo wa mapambano na umoja  katika jamii zote za Kiislamu."

4118714

captcha