IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Maandishi yenye chuki dhidi ya Uislamu yawalenga Wabosnia katika nchi yao

13:10 - February 05, 2023
Habari ID: 3476513
TEHRAN (IQNA) – Michoro yenye chuki dhidi ya Uislamu iliyochorwa huko Capljina nchini Bosnia na Herzegovina ilizua taharuki kutoka kwa wakazi Jumamosi huku polisi wakianzisha uchunguzi kuhusu kesi hiyo.

Makala ya kutisha kama vile "Ua Balija (maneno yanayotumiwa kuwatusi Waislamu wa Bosnia)" na "Tutawachinja Waislamu wanawake na watoto," yaliandikwa kwenye Daraja la Franjo Tuđman huko Capljina, ambapo wanaishi Waksristo wa jamii ya Wakroati.

"Michoro hiyo iliandikwa na watu wasiowajibika ambao wanalenga kuwadhalilisha wakazi wa Bosnia na kueneza chuki, kutovumiliana na migawanyiko kati ya wakazi wa Capljina. Tunatumai kuwa wahalifu hao watapatikana na taasisi tofauti zitakabiliana na tatizo hilo," alisema msemaji wa Utawala wa Jiji Danijela Nogolica.

Aliwataka wakaazi kuwajibika wao wenyewe na kuongeza kuwa serikali ya jiji inalaani kitendo hicho na picha hiyo ilichorwa.

Polisi wa Capljina walisema uchunguzi ulianzishwa ili kuwapata na kuwaadhibu wahusika.

Waharibifu walishambulia msikiti mwishoni mwa juma lililopita kaskazini mashariki mwa Bosnia Herzegovina jambo ambalo lilizua upinzani na ukosoaji mkubwa.

Msikiti wa Dasnica huko Bijeljina ulikojolewa kuta zake na watu wasiojulikana, kwa mujibu wa Bunge la Muungano wa Kiislamu.

3482351

captcha