IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /25

Abdulaziz Ali Faraj; Qari mahiri ambaye hakupata umaarufu

13:31 - February 05, 2023
Habari ID: 3476514
TEHRAN (IQNA) – Abdulaziz Ali Faraj alikuwa qari wa Kimisri ambaye aliishi zama za Ustadh Abdul Basit Abdul Samad.

Abdulaziz Ali Faraj; Qari mahiri ambaye hakupata umaarufuUstadh Faraj alikuwa msomaji mzuri wa Qur'ani Tukufu lakini hakupata umaarufu kama makari wengine kutokana na matatizo fulani.

Alizaliwa mwaka 1927 nchini Misri. Baada ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu, alianza kujifunza usomaji wa Qur'ani na punde akaanza kusoma katika duru na vipindi tofauti vya Qur'ani.

Mwaka 1962 alikuwa miongoni mwa maqkari 170 waliochunguzwa na kamati ya wataalamu kujiunga na Redio ya Qur'ani ya Misri. Alikuwa mmoja wa wasomaji watatu wa Qur'ani waliofaulu mtihani huo.

Ustadh Faraj alikuwa kienda kwenye 'nyumba za kahawa' kila siku. 'Nyumba za kahawa' zilikuwa mahali pa mkusanyiko wa watu wanaopenda utamaduni, sanaa na fasihi. Wasomaji wa Qur'ani Tukufu na Ibtihal pia walikusanyika katika maeneo hayo na walikuwa na majadiliano mazuri kuhusu usomaji wa Qur'ani na sayansi za Qur'ani.

Ustadh Faraj alikuwa miongoni mwa maqari ambao karibu kila siku wangeshiriki katika mijadala hii.

Alikuwa na urafiki mzuri na Abdul Basit Abdul Samad na Mustafa Ismail, maqari wawili mashuhuri wa wakati huo.

Mwishoni mwa maisha yake, Ustadh Faraj alikabiliwa na matatizo mengi ya kifedha kutokana na ugonjwa wake na masuala mengine. Ustadh Abdul Basit ndiye aliyeandaa khitma yake.

Ustadh Faraj, ambaye alikuwa na ulemavu wa macho, alikuwa na sauti yenye nguvu na thabiti. Ni visomo vichache sana vyake vilivyorekodiwa..

Ifuatayo ni qiraa yake ya aya 75-78 za Surah Al-Hajj mnamo 1964.

3482345

captcha