IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /60

Qur'ani inawaonya Waumini kujiepusha na urafiki na makafiri katika Sura Al-Mumtahanah

14:42 - February 05, 2023
Habari ID: 3476515
TEHRAN (IQNA) – Makafiri na maadui wa Mwenyezi Mungu daima wamekuwa wakitafuta kuangamiza dini na kuwaondoa watu katika dini. Wakati fulani hutumia vita na dhuluma na wakati mwingine hunyoosha mkono wa urafiki na kujaribu kuwapotosha waumini kwa njia yoyote wanayoweza.

Ndio maana Mungu anaonya katika Sura Al-Mumtahanah kwamba waumini lazima waepuke urafiki na makafiri.

Al-Mumtahanah ni sura ya 60 ya Qur'ani Tukufu. Ina Aya 13 na iko katika Juzuu 28 ya Kitabu kitukufu. Ni Madani na ni Sura ya 91 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Neno Mumtahanah linarejea kwenye ukweli kwamba baadhi ya wanawake wa Kiislamu walioondoka Makka kwenda Madina walijaribiwa ili kuona lengo lao lilikuwa nini.

Baada ya Hijra ya Mtukufu Mtume (SAW) kutoka Makka kwenda Madina, masahaba zake na Waislamu wengine walikwenda Madina pia. Miongoni mwao walikuwa baadhi ya wanawake waliosilimu. Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume (SAW) awachunguze ili kuona ni nini msukumo wao wa kwenda Madina.

Surah Al-Mumtahanah inazungumzia urafiki baina ya waumini na makafiri na kuupiga marufuku. Aya za mwanzo na mwisho wa Sura zinaonya dhidi ya urafiki na makafiri.

Pia kuna aya kuhusu wanawake ambao wamefanya kiapo cha utii cha Hijra na wanawake na Mtukufu Mtume (SAW).

Sura pia inataja tabia ya Ibrahim (AS) ya kuepuka kuabudu masanamu na kumuomba Mwenyezi Mungu amsamehe baba yake, Azar, kama mfano wa kujiepusha na ukafiri.

Sura inasisitiza kwamba makafiri wananyoosha mkono wa urafiki kwa waumini kwa lengo la kuwapoteza kutoka kwenye Njia Iliyo Nyooka.

Kwa sababu hawana imani na akhera na hawana matumaini nayo, hawawezi kuwa marafiki wazuri kwa Waislamu.

Habari zinazohusiana
captcha