IQNA

Mashindano ya Qur'ani Misri

Misri yazindua Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu

15:12 - February 05, 2023
Habari ID: 3476516
TEHRAN (IQNA) - Toleo la 29 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Misri yalianza katika sherehe katika mji mkuu Cairo siku ya Jumamosi.

Waziri wa Wakfu wa Misri, Sheikh Mohamed Mukhtar Gomaa, alihutubia sherehe za ufunguzi na kulitaja tukio hilo kuwa ni la kipekee la Qur'ani Tukufu linaloimulika Misri na dunia nzima.

Alisema mashindano hayo yanafanyka mjini Cairo na yataendelea hadi Jumatano, Februari 8.

Amebainisha kuwa programu kadhaa za Qur'ani Tukufu zitafanyika pembezoni mwa mashindano hayo, zikiwemo programu za kisomo cha Ibtihal na duru za Qur'ani zinazohudhuriwa na maqari wakuu wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Sheikh Jaber Tayi, afisa wa zamani wa wizara ya Awqaf, pia alizungumza katika hafla hiyo, akisema wagombea 108 kutoka nchi 58 wanashiriki katika mashindano ya kimataifa.

Alibainisha kuwa zawadi za pesa taslimu ambazo zitatolewa kwa washindi wa shindano hilo mwaka huu zimeongezeka maradufu ikilinganishwa na zile za toleo la awali.

Vile vile amepongeza ushiriki wa wawakilishi kutoka nchi zisizo za Kiarabu kama ishara ya kuenea kwa Uislamu na Qur'ani Tukufu duniani.

Kategoria za shindano zinalenga katika kuhifadi Qur'ani nzima, tafsiri, na dhana za Qur'ani.

Kundi la kwanza ni kuhifadhi Quran na kuelewa dhana zake kwa wanaume na wanawake walio chini ya umri wa miaka 45. Mshindi wa kwanza na wa pili watapata Pauni 250,000 na 150,000 za Misri mtawalia.

Kundi la pili ni kuhifadhi Quran na ufahamu wake kwa familia. Angalau watu watatu wa kila familia wanapaswa kuwa wahifadhi Qur'ani. Familia bora itatunukiwa Pauni 250,000 za Misri.

Kundi la tatu ni kuhifadhi, kufasiri na matumizi ya Qur'ani Tukufu katika sayansi nyinginezo kwa washiriki walio chini ya umri wa miaka 45. Pauni 150,000 za Misri zitatolewa kwa mshindi.

Kuhifadhi Qur'ani kwa qiraa saba kwa washiriki walio chini ya umri wa miaka 50 ni kategoria inayofuata yenye zawadi ya juu ya Pauni 150,000 za Misri.

Kundi la tano ni la kuhifadhi Qur'ani kwa wasiozungumza Kiarabu walio chini ya umri wa miaka 40 na zawadi ya juu ya Pauni 150,000 za Misri. Hafidh aliyeshika nafasi ya pili atapata Pauni 100,000 za Misri.

Kundi linalofuata ni kuhifadhi Quran kwa watu wenye ulemavu. Washiriki wanapaswa kuwa na umri wa chini ya miaka 35 kwani mshindi wa kwanza ataleta Pauni 100,000 za Misri.

Kundi la saba ni la kuhifadhi Quran na kuelewa msamiati na tafsiri yake kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 15. Pauni 100,000 za Misri zitatolewa kwa mshindi.

Kategoria ya mwisho imejitolea kwa wakariri wa mfano. Zawadi za juu katika baadhi ya kategoria zimeongezeka hadi Pauni 250,000 za Misri. Thamani ya chini ya tuzo ya juu ni Pauni 100,000 za Misri. Tukio la mwaka huu limepewa jina la marehemu qari Sheikh Mustafa Ismail.

4119713

 

captcha