IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 9 ya Qur'ani ya Ulaya kufanyika Mwezi Machi

16:07 - February 05, 2023
Habari ID: 3476517
TEHRAN (IQNA) – Toleo la tisa la mashindano ya Qur’ani ya Ulaya yanapangwa kufanyika Machi 2023.

Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Taasisi ya Dar-ol-Quran ya Ujerumani, yenye uhusiano na Kituo cha Kiislamu cha Hamburg.

Kulingana na tangazo la awali, mashindano hayo yatafanyika Machi 10-12.

Fainali ya toleo la nane la hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa Aprili 2022 na washindi walipokea tuzo zao mapema Mei.

Usomaji wa Qur'ani, Tarteel, kuhifadhi, tafsiri na dhana za Qur'ani, Adhana, na Qasidah zilikuwa kategoria za mashindano yam waka jana.

Waislamu kutoka shule zote za Kiislamu wanaoishi katika nchi za Ulaya wanaweza kushiriki katika mashindano hayo.

Mashindano hayo ya kila mwaka yanalenga kukuza utamaduni na mafundisho ya Qur'ani, kubainisha na kukuza vipaji vya Qur'ani, na kuimarisha umoja katika jumuiya ya Qur'ani ya Ulaya.

4119800

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu hamburg
captcha