Sheikh Ekrima Sa'id Sabri ametangaza leo kuwa ni wajibu kwa Waislamu na hasa Wapalestina kuitumia fursa wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuhudhuria muda wote katika msikiti wa Al Aqsa ili kukabiliana na njama za Wazayuni. Sheikh Ekrima Sa'id Sabri ameongeza kuwa hivi sasa msikiti wa al-Aqsa unakabiliwa na hujuma kubwa zaidi na uvamizi wa walowezi wa Kizayuni na askari wa utawala wa Kizayuni kuliko ilivyokuwa wakati mwengine wowote ule, hivyo Waislamu na Waarabu wanapaswa wasimame imara kukabiliana na ubeberu wa utawala haramu wa Israel. Kila mara askari na walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakitumia visingizio mbalimbali kuuvamia msikiti mtukufu wa al- Aqsa, ambapo mbali na kufanya uharibifu katika sehemu muhimu za msikiti huo wanawawekea vizuizi mbali mbali Wapalestina ili wasiweze kuingia msikitini humo.../mh