IQNA

Watetezi wa Quds Tukufu

Wanachuo wa Mauritania wapinga uhusiano na utawala haramu wa Israel

20:53 - September 23, 2023
Habari ID: 3477643
TEHRAN (IQNA)- Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Mauritania wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Nouakchott, wakilaani kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Waarabu na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Jumapili iliyopita, walowezi wa Kizayuni waliuvamia tena Msikiti wa Al-Aqsa huku wakisindikizwa na kupewa ulinzi na askari usalama na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kwa mnasaba wa kile kinachoitwa "siku ya kwanza ya mwaka wa Kiebrania".
 
Kwa mujibu wa taarifa, Jumuiya ya Ubunifu wa wanachuo wa Mauritania imeandaa maandamano yaliyoishia mbele ya Msikiti wa Saudia ulioko mjini Nouakchott kupinga mpango na hatua ya  baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Israel, na vilevile kuiunga mkono Baitul Muqaddas (Jerusalem) na Msikiti wa Al-Aqsa.
Wakiwa wamebeba bendera ya Palestina, wanachuo hao waliokusanyika mbele ya msikiti wa Saudia wamelaani hujuma na uvamizi wa kila siku unaofanywa na Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa na kuvunjiwa heshima kibla hicho cha kwanza cha Waislamu.
Aidha, washiriki wa mjumuiko huo wamesifu na kupongeza msimamo wa Mauritania wa kuunga mkono kadhia ya Palestina ikiwa ndio kadhia kuu ya Umma wa Kiarabu na Kiislamu na kuzitaka nchi zote za Kiislamu na Kiarabu zifanye juhudi za kuikomboa ardhi ya Palestina.
Katika mjumuiko wao huo wa kuipinga Israel, wanafunzi wa vyuo vikuu vya Mauritania wamesisitiza pia kuwa: Baitul Muqaddas na Msikiti wa Al-Aqsa ni amana na kuanzisha uhusiano na utawala wa Israel ni uhaini na usaliti.
3485282
Habari zinazohusiana
captcha