IQNA

Msisimko katika hatua ya nusu fainali ya Tilawa ya kuiga

IQNA - Hatua ya nusu fainali ya tamasha la kwanza la Tilawa ya Qur'ani Tukufu ya kuiga ilimalizika jioni ya Ijumaa, Machi 18, kwa visomo maridadi vya wasomaji vijana wa Kiirani. Katika hafla hii, Abolfazl Faraji kutoka Tehran katika kikundi cha umri chini ya miaka 17 aliwavutia wengi katika ukumbi wa mashindano kwa qiraa ya mtindo wa Ustadh Abdul Basit.

Mashindano hayo yanafanyika katika Haram tukufu ya Imamzadeh Saleh (AS) kaskazini mwa Tehran.

Kuna kategoria mbili za umri wa miaka 17-22 na 12-16, huku washindani 32 na 51 wakifika hatua hii katika kila kategoria mtawalia.