IQNA – Polisi wa McKinney, Texas, walifika wiki hii katika eneo la tukio la uhalifu lililotokea katika kituo cha elimu ya Kiislamu ambacho kikundi cha kutetea Waislamu kimekitaja kuwa ni unyanyasaji wa chuki dhidi ya Uislamu.
IQNA – Polisi wa utawala wa Israel wamemkamata Sheikh Mohammad Sarandah, khatibu wa Msikiti wa Al-Aqsa, muda mfupi baada ya kutoa hotuba ya Ijumaa, kwa mujibu wa Waqfu wa Kiislamu wa al-Quds.
IQNA – Mwanaharakati kutoka Malaysia amesema kuwa mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuangazia mambo yanayowafungamanisha na kushikamana kukabiliana na changamoto za pamoja.
IQNA – Mufti Mkuu wa Misri amesisitiza kuwa Qur’ani Tukufu haioni tofauti kati ya mataifa na tamaduni kuwa chanzo cha mizozo, bali huzitambua kama fursa ya ushirikiano na maelewano.
IQNA – Waasi wa RSF wametekeleza shambulizi la ndege isiyo na rubani dhidi ya msikiti mjini el-Fasher, Sudan, siku ya Ijumaa, na kuwaua zaidi ya raia 70, kwa mujibu wa Baraza la Uongozi la Sudan na waokoaji wa eneo hilo.
IQNA – Mamlaka Kuu ya Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu imetangaza mafanikio ya utekelezaji wa mazingira ya kidijitali katika Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume (SAW) mjini Madina.
IQNA – Harakati za mapambano ya ukombozi wa Wapalestina, Hamas na Jihad ya Kiislamu, zimetoa matamko ya kulaani hatua ya Marekani kutumia kura ya turufu au veto kuzuia kupitishwa kwa rasimu ya azimio la kusitisha vita Gaza, wakisema kuwa hatua hiyo inachochea jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
IQNA – Sheikh Abdullah Daqaq, Mkurugenzi wa Chuo cha Kiislamu cha Bahrain kilichoko Qom, amesema kuwa Mtume Muhammad (SAW) ni rehema kwa wanadamu wote, na kwamba umoja wa kweli katika ulimwengu wa Kiislamu unategemea kushikamana na mafundisho yake.
IQNA – Katikati ya vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelea na mashambulizi yasiyokoma ya Israel dhidi ya Gaza, watoto wa Kipalestina waliopoteza makazi wanapata faraja kwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu ndani ya kambi za wakimbizi.
IQNA – Hatua ya mwisho ya mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu imeanza Alhamisi katika mji mkuu wa Afrika Kusini, ikiwakutanisha washiriki kutoka nchi 29.
IQNA – Harakati ya Muqawama au Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah imetangaza ratiba ya shughuli za kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa viongozi wake mashuhuri, Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashem Safieddine.
IQNA – Sheikh Maan bin Ali al-Jarba, Mwenyekiti wa Umoja wa Makabila ya Waarabu wa Iraq, amesema kuwa Sira ya Mtume Muhammad (SAW) inatoa mafunzo muhimu kuhusu umoja na uongozi unaoheshimu haki za raia wote.
IQNA – Maandalizi ya toleo la 28 la Tuzo ya Qur’ani na Sunna ya Sharjah (1447H / 2025) yameanza rasmi katika mji wa Sharjah, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
IQNA – Waislamu wawili kati ya watatu nchini Ufaransa wanasema wamekumbwa na tabia za kibaguzi, kwa mujibu wa utafiti mpya unaoangazia ubaguzi mpana katika ajira, makazi, na huduma za umma.
IQNA – Mwenyekiti wa Baraza la Wasomi wa Rabat Muhammadi nchini Iraq amesema kuwa umoja wa Kiislamu sasa ni jambo la lazima kutokana na changamoto nzito zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu.