IQNA

Allamah Sistani: Acheni fitina za kimadhehebu Iraq

18:04 - June 16, 2014
Habari ID: 1418402
Ayatullah Ali Sistani, kiongozi mkuu wa kidini wa Waislamu wa Kishia nchini Iraq amewataka raia wa nchi hiyo kujiepusha na aina yoyote ya hatua za kidini au ukabila zinazoweza kuvunja umoja wao sambamba na kuacha matumizi ya silaha kinyume cha sheria.

Allamah Sistani amesema na hapa ninamnukuu: “Ni lazima kwa wananchi na hususan katika maeneo ya mchanganyiko, wawe makini katika kuzidhibiti nafsi zao katika kipindi hiki nyeti, wazidishe mapenzi baina yao na kuacha kila aina ya hatua zinazoweza kuzusha fitina.” Mwisho wa kunukuu. Wakati huo huo serikali ya Baghdad imetangaza habari ya kuuawa magaidi 279 katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ndani ya masaa 24 yaliyopita na kwamba, hali ya mambo mjini Baghdadi ni ya kuridhisha. Fariq Qasim, msemaji wa jeshi la Iraq amewambia waandishi wa habari kwamba, jeshi linafanya jitihada za kurejesha hali ya usalama nchini sambamba na kuyakomboa maeneo yote ambayo yanadhibitiwa na magenge ya kigaidi. Naye kwa upande wake Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki, amesema kuwa, operesheni za kuyakomboa maeneo yanayodhibitiwa na Daesh, zitaanza hivi karibuni.

1417153

Kishikizo: sistani iraq daesh
captcha