IQNA

Meya aliyetusi Uislamu wa Ufaransa akataa kufika mahakamani

19:50 - June 25, 2014
Habari ID: 1422665
Meya wa eneo la 16 la Paris ambaye mapema mwaka huu hakuhudhuria mahakamani kwa kosa la kuvunjia heshima Uislamu, amekataa tena kufika mahakamani kwa mara pili.

Meya Claude Goasguen alishtakiwa katika mahakama ya mji wa Nimes mapema mwaka huu kwa tuhuma ya kuvunjia heshima Uislamu kufuatia mashtaka yaliyowasilishwa na Tasisi ya Kitaifa ya Kusimia Wimbi la Kuhujumu Uislamu ya Baraza la Waislamu la Ufaransa.
Wakili wa Meya huyo ambaye alifika mahakamani badala ya mteja wake amedai kwamba matamshi yake hayakuakisiwa ipasavyo.
Mahakama ya Nimes imeainisha tarehe 11 Septemba kwa ajili ya kikao cha tatu cha kesi inayomkabili meya huyo wa Ufaransa. Mwezi Februari mwaka huu Meya huyo wa eneo la 16 la Paris alihutubia mkutano wa Mayahudi akidai kuwa vijana wa Kiislamu wanarubuniwa misikitini ili wakanushe uhakika wa mambo kuhusu Mayahudi. Meya huyo anahukumiwa kwa tuhuma za kueneza ubaguzi na chuki dhidi ya Waislamu.   1422345

Kishikizo: Waislamu, Meya, ufaransa
captcha