IQNA

Waziri Mkuu wa Iraq ni mwalimu na msomi wa Qur'ani

10:54 - August 14, 2014
Habari ID: 1439232
Waziri Mkuu mteule wa Iraq Haider al—Abadi ni msomi mashuhuri wa Qur'ani.

Abadi ambaye anachukua nafasi ya waziri mkuu anayeondoka Nouri al-Maleki ameandika vitabu kadhaa na makali kuhusu Uislamu na Qur'ani.
Aidha alifundisha taalamu ya sayansi za Qur'ani na Tafsiri katika Chuo Kikuu cha Sayansi za Qur'ani mjini London kuanzia mwaka 1999 hadi 2003.
Abadi alizaliwa Baghadad mwaka 1952 na kuendelekza masomo yake ya juu katika Chuo Kikuu cha Baghdad. Baadaye alielekea Uingereza katika Chuo Kikuu cha Manchester ambapo alihitimu kwa shahada ya uzamivu (Phd). Aliishi uhamishoni Uingereza na familia yake kutokana na kuwa alikuwa kati ya wapinzani waliokuwa wamelengwa kuuawa na utawala wa kiimla wa chama cha Baath cha Saddam Hussein. Abadi aliwahi kuwa msemaji wa muda mrefu wa Chama cha Daawa ya Kiislamu cha Iraq.
Siku ya Jumatatu Rais mpya wa Iraq Fouad Masoum amemtea naibu spika wa Bunge  kuwa waziri mkuu  wa nchi hiyo. Massoum amempa siku 30 Haidar al Abadi kuunda serikali mpya na kuiwasilisha bungeni ili ipitishwe.
Muda mfupi baada ya kuteuliwa, al Abadi alitoa wito wa kuimarishwa umoja dhidi  ya mashambulizi ya  kundi la kigaidi la ISIL nchini humo.

1439021

Kishikizo: iraq abadi qur'ani
captcha