IQNA

Mufti Mkuu wa Tunisia asema ISIS ni tishio kuu kwa ulimwengu wa Kiislamu

12:31 - October 17, 2015
Habari ID: 3386403
Mufti Mkuu wa Tunisia amesema kuwa mirengo yenye kufurutu ada na makundi ya kitakfiri kama ISIS au Daesh ni tishio kuu kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Sheikh Hamda Said amesema wale wote wanaowasaidia matakfiri kwa hakika wanahudumia maslahi ya utawala bandia wa Israel ili kusahahaulisha kadhia ya Palestina. Mufti Mkuu wa Tunisia ameyasema hayo katika mazungumzo aliyofanya na Sheikh Muhammd Asadi Muwahhed Mkuu mpya wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran nchini Tunisia. Mufti Mkuu wa Tunisia amezilaani baadhi ya nchi za Kiislamu kwa kunyamaza kimya mbele ya jinai za Israel na kuongeza kuwa, maulamaa wa Kiislamu wana jukumu la kuuchambua wazi wazi utawala wa Kizayuni unaoikalia Quds kwa mabavu.  Katika mazungumzo hayo, Sheikh Muhammad Asadi Muwahhed pia amesema, sababu kuu ya kuwepo hitilafu ni ujinga na kutofahamu na kwamba, hitilafu zitapungua iwapo Waislamu na madhehebu ya dini hiyo watafanya mazungumzo bila ya taasubi na kutambua kikamilifu na kwa usahihi dhehebu la kila mmoja.

3386124

captcha