IQNA

Waislamu Japan wafanyiwa ujasusi na polisi

23:15 - August 06, 2016
Habari ID: 3470498
Polisi huko Tokyo nchini Japan wanawafanyia ujasusi Waislamu kwa sababu ya dini yao, tokea mwaka 2008.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mahakama Kuu ya Japan imetupilia mbali kesi iliyokuwa imewasilishwa kuhoji msingi wa sheria katika ujasusi huo wanaofanyiwa Waislamu Wajapani. Hii ni katika hali ambayo kumpeleleza mtu kwa sababu ya dini au kabila lake ni kinyume cha sharia kwa mujibu wa Katiba ya Japan ambayo inasisitiza haki ya faragha na kulindwa wote na sheria sambamba na wote kupata kinga sawa ya kisheria na uhuru wa kuabudu.

Ilibainika kwa mara ya kwanza mwaka 2010 kuwa polisi mjini Tokyo wana kitengo maalumu cha kuwapeleleza kwa siri Waislamu. Nyaraka zilizofichuka zinaonyesha majina ya Waislamu 72,000 wanaochunguzwa kwa siri na polisi nchini Japan.

Imebainika kuwa polisi Japan waliweka kamera za siri ndani ya misikiti au kutumia makachero waliojipenyeza katika mashirika ya misaada ya Kiislamu, bucheri na migahawa ya Waislamu.

Inakadiriwa kuwa kuna Waislamu wapatao laki moja nchini Japan ambapo baadhi ni wenyeji wa nchi hiyo huku wengine wakiwa ni wanafunzi au raia wa kigeni waliopata idhini ya kuishi daima nchini humo.

3460610

Kishikizo: waislamu japan misikiti
captcha