IQNA

Ongezeko kubwa la Hujuma za Chuki Dhidi ya Uislamu Marekani

19:39 - October 23, 2016
Habari ID: 3470630
IQNA-Uhalifu na hujuma zitokanazo na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) umeongezeka kwa asilimia 89 nchini Marekani.

Takwimu mpya za kitaifa zinaonyesha kuwa, kumekuweko na ongezeko kubwa la hujuma na uhalifu nchini Marekani ambao chimbuko lake ni chuki dhidi ya Waislamu. Ripoti iliyotolewa na mtandao wa gazeti la Huffington Post inaonyesha kuwa, baada ya kufanyika uchunguzi katika majimbo 20 ya Marekani na katika mji wa New York imefahamika kwamba, uhalifu dhidi ya Waislamu unaotokana na chuki dhidi ya wafuasi wa dini hiyo umeongezeka.

Utafiti huo ambao unatarajiwa kukabidhiwa kwa Shirika la Kutambua Uhalifu la Marekani, unaonyesha kuwa, kiujumla uhalifu unaotokana na chuki umeongezeka kwa asilimia 6 nchini Marekani ilihali uhalifu unaowalenga Waislamu umeongezeka kwa asilimia 89.

Kwa mujibu wa utafiti huo, uhalifu unaotokana na chuki katika mji wa New York pekee umeongezeka kwa asilimia 24.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa, vita nchini Syria, matangazo na video za kutisha za kundi la kigaidi la ISIS au Daesh zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii zimekuwa na nafasi kubwa katika kuongeza hisia za chuki dhidi ya Waislamu katika jamii ya Wamarekani.

Infaa kuashiria hapa kuwa, kufuatia tukio la Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani, kuliibuka wimbi jipya la chuki dhidi ya Waislamu katika jamii ya Marekani na hivyo kuathiri pakubwa maisha ya Waislamu katika nchi hiyo.

Aidha wimbi jipya la chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia limeshuhudiwa katika nchi za Maghairbi baad aya hujuma kadhaa za kigaidi huko Ulaya na Marekani ambapo wanaotekeelza uhalifu huo hujifungamanisha na Uislamu. Hii ni pamoja na kuwa viongozi wa Kiisalmu na Waislamu waliowengi hutangaza kulaani hujuma kama hizo za kigaidi.

3539955.


captcha