IQNA

Facebook yafuta kwa makusudi akaunti za Wanaharakati wa Palestina

22:07 - October 26, 2016
Habari ID: 3470636
IQNA-Mtandao wa kijamii wa Facebook unalaumiwa kwa kufuta akaunti za wanaharakati na waandishi habari wanaopinga utawala haramu wa Israel na kutetea ukombozi wa Palestina.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, shirika moja la kutetea haki za Wapalestina mbali na Facebook kufunga akaunti hizo, katika kipindi cha mwaka moja uliopita, idadi kubwa ya wanaharakati na waandishi habari wamekamatwa na kufungiwa katika jela za Israel kutokana na maandishi yao katika mitandao ya kijamii.

Mousa Rimawi, Mkurugenzi wa Kituo cha Palestina cha Kustawisha Uhuru wa Vyombo vya Habari (MADA) amechapisha ripoti kuhusu kukandamizwa waandishi habari wa Wapalestina mikononi mwa maafisa wa utawala dhalimu wa Israel.

Ameongeza kuwa, wakuu wa utawala haramu wa Israel wanayashinikiza mashirika ya mitandao ya kijamii kama Facebook kufuta maandishi yoyote yaliyo dhidi ya utawala wa Tel Aviv. Itakumbukwa kuwa, mwezi Septemba, ujumbe wa Facebook ulikutakana na maafisa wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ajili ya mazungumzo ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Israel Gilad Erdan aliyataja kuwa yaliyofanikiwa.

Wiki hii wanaharakati wa Kituo cha Habari cha Palestina (PIC) walisema akaunti zao 10 za lugha za Kiarabu na Kiingereza katika Facebook, ambazo zilikuwa na wafuasi zaidi ya milioni mbili, zimefungwa kwa muda au kufungwa daima. Hatua hiyo ya kubana uhuru wa maoni imechukuliwa baada ya maafisa wa Facebook kutembelea Israel.

Ikumbukwe kuwa Mark Zuckerberg, mwanzilishi mwenza wa tovuti ya kijamii ya Facebook ni Yahudi ambaye amekuwa akishirikiana na wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Itakumbukwa kuwa, miaka 68 iliyopita, utawala bandia wa Israel ulitangaza uwepo wake baada ya kufanya mauaji makubwa ya umati dhidi ya Wapalestina. Askari wa Uingereza waliikalia kwa mabavu Palestina kufuatia kushindwa utawala wa Othmania wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia. Miaka mitano baadaye Jumuiya ya Kimataifa ikaibidhi Palestina kwa Uingereza na kuifanya chini ya mamlaka ya mkoloni huyo. Novemba mwaka 1947 Umoja wa Mataifa ukapasisha azimio lililotaka kuundwa madola mawili ya Kiarabu na Kiyahudi huko Palestina.

Tokea wakati huo Wapalestina wamekuwa wakipigana kuzikomboa ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na Palestina.

3461249/

captcha